Dar es Salaam — Tanzania na Umoja wa Ulaya wamesaini Mkataba wa Msaada wa Kilimo (Agricultural Support Agreement) wenye thamani ya euro milioni 180 (shilingi bilioni 540), ukilenga kuimarisha kilimo cha kisasa na usalama wa chakula nchini Tanzania kwa kipindi cha miaka 5.

Mradi huu, unaojulikana kama "Tanzania Agricultural Transformation Programme" (TATP), utajumuisha upatikanaji wa teknolojia bora za kilimo kwa wakulima wadogo, ujenzi wa mifumo ya umwagiliaji, na mafunzo ya kisayansi kwa wakulima zaidi ya 500,000.

Balozi wa EU Tanzania, Manfredo Fanti, alisema: "Tunaamini kwamba Tanzania ina uwezo mkubwa wa kuwa ghala la chakula la Afrika. Msaada huu unaelekeza nguvu zetu katika sekta muhimu zaidi — kilimo cha wakulima wadogo."